Shirika la ndege la flydubai limetangaza njia tatu nchini Tanzania


(MENAFNEditorial) DAR ES SALAAM Tanzania September 23 2014/African Press Organization (APO)/ -- Shirika la ndege lenye makao yake Dubai leo limetangaza uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam Zanzibar na Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari za ndege za nchi hii ya Afrika Mashariki zitaanza Oktoba zikikuza mtandao wa shirika hili la ndege barani Afrika hadi vituo 12.

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/flydubai.jpg

Photo 1: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1388 (Ghaith Al Ghaith Chief Executive Officer of flydubai)

Photo 2: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1297 (flydubai fleet)

Photo 3: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1389 (Sudhir Sreedharan Senior Vice President Commercial (GCC Subcontinent and Africa)

Photo 4: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1298 (flydubai Business Class)

Photo 5: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1387 (Economy seats)

Photo 6: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1295 (flydubai Business Class Lounge)

Photo 7: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1386 (Downtown Burj Khalifa)

Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa safari hizi Ghaith Al Ghaith Afisa Mkuu Mtendaji wa flydubai (http://www.flydubai.com) alisema: "Kwa kuongeza safari hizi tatu mpya nchini Tanzania tumekuza mtandao wetu mara mbili katika Afrika ya Kaskazini na Mashariki mwaka huu tukiimarisha ahadi yetu ya kuhudumia masoko ambayo hayakuhudumiwa vya kutosha."

Hivi karibuni flydubai ilitangaza uzinduzi wa safari za ndege za Bunjumbura nchini Burundi Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda na safari za vituo hivi zitaanza mwishoni mwa Septemba.

Tanzania ni kitovu cha eneo upande wa utalii wa Afrika Mashariki na mwakani 2013 nchi hiyo iliwakaribisha watalii milioni 1. Kulingana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) idadi hii inatarajiwa kuongezeka mara mbili na watalii milioni 2 wakitarajiwa ifikapo 2017.

Makamu Mkuu wa Rais wa Biashara Sudhir Sreedharan (GCC Bara Dogo na Afrika) alisema "Mtandao wetu unaoendelea kukua unaunga mkono Dira ya Utalii ya 2020 ya Dubai inayolenga kuwavutia wageni milioni 20 katika Umoja wa Falme za Kiarabu ifikapo 2020.

Kwa kutoa huduma za kuaminika kwa bei nafuu na zilizo rahisi za usafiri kutoka Tanzania tunawapa abiria fursa ya kusafiri Dubai na kuunganisha safari zao na zaidi ya vituo 200 duniani kote kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai."

Tanzania ni nchi inayojulikana kwa uzuri wake wa asili na wanyamapori. Dar es Salaam ni kitovu cha biashara nchini Tanzania na mji huo una bandari linalovutia na vivutio tele vya kitamaduni na kihistoria. Unguja inayojulikana kama Kisiwa cha Viungo imefunikwa na pwani nyeupe na imejaa utamaduni historia na wanyamapori wanaopatikana huko tu. Zaidi ya hayo vilele vya Mlima Kilimanjaro vilivyofunikwa na theluji huwakaribisha watalii kwa matembezi na kuteleza juu ya theluji mwaka mzima.

flydubai imeunda mtandao mpana barani Afrika ulio na safari za ndege za Addis Ababa nchini Uhabeshi Alexandria nchini Misri Khartoum na Port Sudan nchini Sudani Djibouti mji mkuu wa Djibouti Juba nchini Sudani Kusini pamoja na Bujumbura nchini Burundi Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda.

Maelezo ya Safari za Ndege"

Dar es Salaam

flydubai itaendesha safari za ndege kila siku kati ya Dubai na Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 Oktoba 2014.

FZ670 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:20 machana saa za ndani itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:55 jioni saa za ndani.

FZ672/674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 12:20 jioni saa za ndani itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani.

FZ669/671/673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:20 asubuhi saa za ndani.

Nauli za safari ya pande zote

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

Kilimanjaro kupitia Dar Es Salaam

flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Kilimanjaro na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 17 Oktoba 2014.

Jumatatu na Ijumaa:

FZ674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 10:10 jioni saa za ndani itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

FZ673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 7:25 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

Nauliza pande zote mbili

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kilimanjaro hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

Zanzibar kupitia Dar Es Salaam

flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Unguja na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 19 Oktoba 2014.

Jumanne na Jumapili: FZ672 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 9:40 mchana saa za ndani itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

FZ671 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani iwasili Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 7:05 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

Nauli za safari ya pande mbili

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Unguja hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

Tiketi za safari hizo za ndege zinaweza kununuliwa kuanzia leo kutoka tovuti ya flydubai (flydubai.com) Kituo chake cha Simu cha ndani +255 (22) 2124005 maduka ya usafiri ya flydubai au kupitia wabia wa usafiri. Taarifa na maelezo zaidi ya huduma za shirika hili za ukodishaji gari na bima ya safirini pia zinaweza kupatikana kwenye flydubai.com.

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of flydubai.

Media contact:

Houda Al Kaissi

Senior Press Officer

t. +971 4 603 3073

m. +971 56 683 0336

news@flydubai.com

Kuhusu flydubai:

Shirika la ndege lenye makao yake Dubai linajikakamua kuondoa vizuizi vya usafiri na kuimarisha uhusiano kati ya tamaduni tofauti katika mtandao wake unao endelea kukua. Tanug uzinduzi wa biashara yake mnamo 2009 flydubai (http://www.flydubai.com):

• Imeunda mtandao wa vituo 83 pamoja na safari 20 mpya zilitangazwa 2014.

• Imefungua safari 53 mpya ambazo hapo awali hazikuwa na safari za moja kwa moja hadi Dubai au hazikuwa zinahudumiwa na shirika la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu kutoka Dubai.

• Imeunda msafara wa ndege 40 mpya na inasubiri kuwasilishwa kwa zaidi ya ndege 100 ifikapo mwisho wa 2023.

Zaidi ya hayo wepesi na urahisi wa flydubai kama shirika changa la ndege umeimarisha ukuaji wa uchumi wa Dubai kufuatana na dira ya Serikali ya Dubai kwa kuanzisha mtiririko wa biashara na utalii katika masoko ambayo hayakuwa na huduma hizi.

For more information about flydubai services please visit http://www.flydubai.com.


Legal Disclaimer:
MENAFN provides the information “as is” without warranty of any kind. We do not accept any responsibility or liability for the accuracy, content, images, videos, licenses, completeness, legality, or reliability of the information contained in this article. If you have any complaints or copyright issues related to this article, kindly contact the provider above.